HOMA YA INNI

Homa ya ini(Hepatitis b) Ni virusi vinavyoenea katika ini na kusababisha madhara makubwa katika ini. Ini ni kiungo muhimu mwilini na kazi yake ni kusaga vyakula pamoja na kemikali zinazoleta madhara, kutengeneza protini na kuhifadhi vitamin muhimu, madini na sukari

Posted  109,804 Views updated 8 months ago

HOMA YA INNI

HOMA YA INNI 

Homa ya ini(Hepatitis b) Ni virusi vinavyoenea katika ini na kusababisha madhara makubwa katika ini. Ini ni kiungo muhimu mwilini na kazi yake ni kusaga vyakula pamoja na kemikali zinazoleta madhara, kutengeneza protini na kuhifadhi vitamin muhimu, madini na sukari

Huu ni ugonjwa ambao unasababishwa na virus ambao hushambulia inni waitwao HEPATITIS B VIRUS, C or A (HBV,  HCV, HAV). Kwa Tanzania watu wengi walioathirika na ugonjwa huu umesababishwa na virus aina ya HEPATITIS B. Idadi ya waathirika wa ugonjwa huu inaendelea kuongezeka siku hadi siku. Ugonjwa huu ni hatari kuliko VVU kwani wagonjwa wa homa ya Ini hufariki dunia mapema ukilinganisha na wa VVU. Pia uwezekano wa kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni mara 100 ukilinganisha na VVU.

Kuna watu kadri ya milioni 350 duniani, ambao wameambukizwa na ugonjwa huu wa hepatitis B na ugonjwa huu unazidi kila siku

KUENEA KWA HOMA YA INI

Hepatitis B ni virusi vilivyopo katika damu na katika majimaji ya miili ya wagonjwa. Ni ugonjwa unaosambaa kirahisi. Huambukizwa kwa njia tofauti kama vile:-

§  Kujamiana na mtu aliyeathirika na ugonjwa huu bila kondomu (ngono kati ya mwanamke/mwanamme na mwanamme/mwanamme ). Hii ni hatari kwa sababu majimaji ya mwili yanaweza kuwa na virusi.

§  Kuchangia miswaki,mashine ya kunyolea au vifaa vya kuchorea mwili na vya kutoboa ngozi visivyotakaswa vizuri

§  Kuchangia nguo au taulo na mwathirika

§  Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hasa wakati wa kujifungua

§  Kugusa majimaji kutoka kwa mtu aliyeathirika mfano damu, jasho, mate, mkojo

DALILI ZA HOMA YA INI

§  Kukosa hamu ya kula na kupungua uzito

§  Macho au ngozi kuwa ya njano

§  Choo kuwa cha kijivu

§  Kutokwa na damu kwa urasi hasa wakati wa kupiga mswaki

§  Maumivu ya Tumbo

§  Homa za mara kwa mara

§  Kuumwa kichwa bila mpango

§  Mwili kuchoka na kudhoofika

§  Kichefuchefu

§  Kutapika

§  Kuhara

§  Mkojo  kuwa kama chai ya rangi au wa njano

§  Tumbo kuvimba hasa kwenye hatua ya mwisho

NB:  Idadi kubwa ya watu wenye Hepatitis hawajijui kama wameambukizwa kwa sababu hawaonyeshi dalili zozote. Njia pekee ya kujua kama umeambukizwa na Hepatitis B ni kupima damu ili kugundua uambukizo.

NANI YUKO KATIKA HATARI YA KUAMBUKIZWA?

·         Watoto wanaozaliwa na mama mwenye uambukizo

·         Mweza, mtoto, au mtu anayeishi nyumbani mwenye uambukizo.

·         Watu wanaofanya kazi katika sehemu ambazo wanaweza kushika majimaji ya mwili, kwa mfano madaktari, manesi, daktari wa meno, maafisa wa magereza, au polisi.

·         Mtu anayefanya mapenzi na watu tofauti mara kwa mara, haswa wale ambao hawatumii kondomuu.

·         Mtu  anayejidunga sindano ya madawa ya kulevya na kuchangia vifaa vya kujidunga madawa

TIBA

·         Tiba ya hepatitis B bado haijapatikana ingawa kuna matibabu ambayo yanaweza kusaidia ini lisiendelee kuharibika na virusi visiendelee kuzaliana. Mafanikio ya chanjo yanatofautiana kati ya watu tofauti.

·         Ugonjwa huu ukishafikia kiwango cha ini kuharibika au kupata saratani ya ini, maana yake kinachofatia ni kifo.

CHANJO

§  Kwa mtu ambao siyo waathirika wanahitaji kupatiwa chanjo ya homa ua ini ili kujikinga na ugonjwa huu.

§  Chanjo hii hupewa dozi mara tatu kwa vipindi tofauti. Dozi ya kwanza hadi ya pili huchukua mwezi mmoja na dozi ya pili hadi ya tatu huchukua miezi 6. Baada ya hapo mtu akisha tumia hizo dozi anakuwa tayari ashamaliza chanjo yake.

NAMNA YA KUZUIA KUENEA KWA HOMA YA INI

·         Kuepuka ngono zembe

·         Kuepuka kukutana na majimaji kutoka kwa mtu aliyeathirika na virusi hawa.

·         Kuepuka kuchangia vitu vya ncha kali.

HITIMISHO

·         Siyo watu wote wanaoathiriwa na Hepatitis B Virus wanakuwa waathirika. Zaidi ya asilimia 87 ya watu wanaoathiriwa na virusi hivi mwili huweza kupambana navyo na huweza kutoweka ndani ya miezi mitatu hadi sita.

USHAURI

Mpaka sasa Homa ya ini haina Tiba, ugonjwa huo ukishafikia kiwango cha ini kuharibika au kupata saratani ya ini, maana kinachofuata ni kifo, Hivyo basi ni vyema kumuona dakitari kwa ushauri na uchunguzi zaidi pindi unapojihisi unamiongoni mwa dalili hizo.


Your reaction?

1
LOL
1
LOVED
0
PURE
0
AW
0
FUNNY
0
BAD!
1
EEW
0
OMG!
0
ANGRY
0 Comments