News
7, Jul 2019 08:55 AM
News
9, Sep 2019 09:47 AM
News
10, Oct 2019 08:32 PM
News
8, Aug 2019 08:18 AM

NINI MAANA YA NGUVU ZA KIUME

Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu kama vile pelvic floor, tezi pituitary (pituitary gland

Posted  66,682 Views updated 8 months ago

NINI MAANA YA NGUVU ZA KIUME

NINI MAANA YA NGUVU ZA KIUME

Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu kama vile pelvic floor, tezi pituitary (pituitary gland) nk havifanyi kazi vizuri kama jinsi inavyopaswa.Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homon Fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance ),

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:-

      1.      Kukosa hamu ya mapenzi

      2.      Uume kusimama kwa uregevu

      3.      Kuwahi kufika kileleni

      4.      Kushindwa kurudia tendo la ndoa

      5.      Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

      6.      Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji

      7.      Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu.

Upungufu wa nguvu za kiume ni kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaumem Ikitokea tezi dume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa.

KINACHOPELEKEA VIUNGO VISHINDWE KUFANYA KAZI

      1.      Vyakula tunavyokula

      2.      Tabia na mtindo wa maisha vinaweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri.

      3.      Kujichua/punyeto (masturbation)

      4.      Kisukari pamoja na presha ya kushuka na kupanda

      5.      Unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya

      6.      Kufanya kazi na kukosa muda wa kupumzika

      7.      Kutokunywa maji ya kutosha na kutofanya mazoezi

SABABU ZINGINE

SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER), Matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama  vile mwondoko na balansi(multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya matunda vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k

Maumivu ya mgongo/kiuno baadhi ya madawa ya kemikali I(madawa ya hospitali), kiharusi (stroke), upungufu katika utendaji wa kaziza gonadi (hypogonadism) uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid.

Kutozalishwa kwa homoni ya throid ya kutosha, ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol( cushing’s syndrome), ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease), kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis).

NB: Hivyo mwanaume unapopunguanguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua kwa nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa.Unapopungukiwa nguvu za kiume hiyo ni dalili ya tahadhari kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu hakifanyi kazi vyema. Hivyo unaambiwa chukua TAHADHARI kabla ya HATARI.

KOSA LINALOFANYWA NA WANAUME WENGI

Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu. Hili ni KOSA KUBWA sana.

Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka zaidi ya 100 na hata miaka 1000 na hujapona.

Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung’olewe kwanza!

Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kasha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndo matibabu.

Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanaume au shinikizo la damu la kupanda( high blood pressure) kwa mwanaume yukle au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni(Hormonal imbalance) kwa wanawake wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja?

Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana

Ushauri : Unapoona dalili kama nilizo taja hapo juu na dalili zingine ambazo huzielewi basi nenda hospitali au kituo cha Afya kilicho karibu ili upate Ushauri, vipimo na matibabu.


Your reaction?

1
LOL
0
LOVED
0
PURE
0
AW
0
FUNNY
0
BAD!
0
EEW
0
OMG!
0
ANGRY
0 Comments