News
10, Oct 2019 06:31 PM
News
6, Jun 2019 05:15 PM

UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI/SEHEMU ZA SIRI (VAGINAL THRUSH)

UKE ni kiungo cha uzazi wa mwanamke, ambamo ndani yake kuna Lactobacillus bacteria na fangasi wazuri ambao wako katika kiwango kinacho lingana/a balanced mix.

Posted  35,059 Views updated 8 months ago

UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI/SEHEMU ZA SIRI (VAGINAL THRUSH)

UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI/SEHEMU ZA SIRI  (VAGINAL THRUSH)

UKE ni kiungo cha uzazi wa mwanamke, ambamo ndani yake kuna Lactobacillus bacteria na fangasi wazuri ambao wako katika kiwango kinacho lingana/a balanced mix. Bacteria hawa na fangasi hizi husaidia sana kuulinda uke na maradhi mbalimbali endapo uwiano wake hauta bughuziwa.

Lactobacillus bacteria hutoa acid ambazo huzuia fangasi kukuwa au kuwa wengi zaidi.

UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI

Ni ugonjwa anaoupata mwanamke endapo fangasi watakuwa wengi zaidi ya bacteria wazuri waliopo ukeni au kama pH ya ukeni imezidi kiwango cha kawaida kinachopaswa (Ph 3.5 – 4.5 ndio kiwango kizuri kiafya).

FANGASI WA UKENI

Mara nyingi husababishwa na fangasi waitwao CANDIDA ALBICANS, lakin wakati mwingine husababishwa na aina nyingine za fangasi ambazo huwa ni vigumu sana kutibika kuliko Candida albicans.

SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha ugonjwa huu wa fangasi, lakini baadhi ya hizo ni kama zifuatazo:-

      1.      MATATIZO YA HOMONI(HOMONI ZA KUBADILIKA/KUWA NYINGI SANA AU KUSHUKA)

Hii inaweza kusababishwa na Ukomo wa hedhi, ujauzito, (MP) kuwa katika siku za mwezi, matumizi ya dawa za kuongeza kiwango cha hormone za kike.

      2.      MATUMIZI YA ANTIBIOTICS hizi huuwa bacteria wazuri na kubadiri pH ya uke.

      3.      KUFANYA MAPENZI NA MTU ALIYE NA UGONJWA WA FANGASI ZA SEHEMU ZA SIRI BILA KINGA

      4.      KUSHUKA KWA KINGA MWILINI hii inaweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali kama UKIMWI, KISUKARI, UPUNGUFU WA MADINI, VITAMINI NA VIRUTUBISHI MBALIMBALI VYA MWILI.

      5.      ULAJI MBAYA HASA KUPENDELEA VYAKULA VYENYE SUKARI KWA WINGI( SUKARI NI CHAKULA KWA FANGASI HIVYO HUONGEZEKA)

DALILI ZINAZOONESHA KUWA UNA UGONJWA WA FANGASI ZA UKENI

Kuna dalili nyingi sana kama ifuatavyo:-

·         Muwasho sehemu za siri.

·         Vipele vidogo vidogo ukeni.

·         Kutokwa kwa uchafu mweupe au rangi ya kijivu ukeni wenye harufu mbaya.

·         Vidonda au michubuko ukeni.

·         Kutokwa na harufu mbaya ukeni.

·         Kupatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

·         Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wan je wa uke.

·         Kuwaka moto ndani na nje ya uke.

KINGA ZA FANGASI ZA KIKE

      1.      Epuka kusafisha uke kwa kutumia vitu vyenye kemikali kama vile sabuni.

      2.      Epuka kutumia marashi yenye kemikali ukeni na kuingiza vitu mbalimbali ukeni kama Vidole, asali n.k

      3.      Epuka kutawadha kutokea nyuma kwenda mbele baada ya kujisaidia haja kubwa

      4.      Fanya matibabu kwa mpenzi wako alien a ugonjwa wa fangasi ili kuepuka uenezi wa fangasi zaidi.

      5.      Safisha uke na kujifuta kwa kitambaa safi ili kuuacha mkavu.

      6.      Vaa chupi zilizotengenezwa kwa vitu harisi kama Pamba na Hariri na epuka kununua nguo za ndani za mtumba kama chupi.

      7.      Tumia Pads zisizo na kemikali na zenye vitu vya kukulinda na maambukizi, kukufanya uwe mkavu na huru kama BF Suma Sanitary Pads nk

MATIBABU YA FANGASI ZA KIKE

§  Ukigundua unadalili hizi tulizozitaja hapo au unahisi hali si ya kawaida kwenye sehemu zako za siri basi nenda kituo cha afya kwa ushauri, vipimo na matibabu zaidi.

§  Vipimo ni kitu cha kwanza kabla ya kutumia dawa yoyote na epuka kununua dawa usizojua matumizi yake na si kila muwasho una maanisha unafangasi wakati mwingine ni muwasho wa kawaida ama allergy.

Napenda kuwashauri wanawake kuwa na tabia ya kuchunguza afya yako mara kwa mara ili kuondokana na magonjwa na madhara yasiyo ya lazima.


Your reaction?

5
LOL
2
LOVED
0
PURE
1
AW
0
FUNNY
0
BAD!
0
EEW
0
OMG!
0
ANGRY
0 Comments