News
6, Jun 2019 09:15 PM
News
8, Aug 2019 06:16 PM
News
6, Jun 2019 10:48 PM

UMUHIMU WA VITAMINI A MWILINI

UMUHIMU WA VITAMINI A MWILINI

Posted  70 Views updated 6 days ago

UMUHIMU WA VITAMINI A MWILINI

VITAMINI A NI NINI?
Vitamini A ni moja wapo ya virutubisho muhimu katika kipindi chote cha masiha ya binadamu. Vitamini A huhitajika mwilini kusaidia macho kuona vizuri, ukuaji na maendeleo ya mtOto na kuimarisha kinga ya mwilini dhidi ya maradhi mbalimbali.

Mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza vitamin A, hivyo vitamin A inapatikana kwenye vyakula tu. Aidha vyakula vyenye viatamini A kwa wingi vitokanavo na wanyama, mfano maziwa ya mama na maziwa ya wanyama wengine, mtindi, siagi, jibini, smaki, ini, kiini cha yai na vile vitokanavyo na mimea kama vile, mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi, matunda yenye rangi ya majano, mafuta ya mawese, mazao ya mizizi kaka karoti na viazi vitamu vyenye rangi ya majano.
Lakini pia vitamin A hupatikana kwenye vyakula vilivyoongezewa kirutubishi hiki kwa watoto wachanga na wadogo chanzo bora zaidi cha vitamin A ni maziwa ya mama.

 

KWANINI UPUNGUFU WA VITAMINI A NI TATIZO NCHINI TANZANIA.
Maziwa ya mama ni chanzo pekee cha vitamin A kwa motto kwa miezi 6 ya mwanzo;
· Lakini watoto wachache tu Nchini Tanzania wananyonyesha maziwa ya mama pekee bila kupewa kinywaji au chakula kingine hadi wanapofikia umri wa miezi 6 na kasha kuendelea kunyonyesha maziwa ya mama hadi kufikia umri wa miaka miwili au zaidi.
· Vyakula wanavyopewa watoto wadogo havina vitamin A ya kutosheleza mahitaji yao kwa sababu hula kiasi kidogo cha chakula na familia nyingi hazifahamu vyakula vyenye vitamin A kwa wingi.
· Familia haziwezi kumudu kuwapa watoto wao vyakula vyenye vitamin A kwa wingi.
· Vyakula vya gharama nafuu vyenye vitamin A kwa wingi havipatikani kwa misimu yote katika mwaka
· Vitamini A iliyomo kwenye chakula hupotea wakati wa matayarisho.
· Maradhi kama vile kuharisha, surua na maradhi ya mfumo wa hewa husababisha upungufu wa vitamin A mwilini.

KWA NINI MAAMBUKIZI YA MINYOO NI TATIZO NCHINI TANZANIA?
· Maambukizi ya minyoo hutokea kwa kula chakula chenye minyoo hai au manyai ya minyoo (kama vile kachumbari) au kissichopiwa vya kutosha.
· Kunywa maji ya kunywa yenye minyoo hai au mayai ya minyoo au maji yasiyochemshwa.
· Kutembea bila viatu au kuchezea udongo uliochafuliwa na kinyesi
· Uchafuzi wa mwili na mazingira, hasa kwa mtayarishaji na vyombo vya kulia chakula na mazingira ya kulia chakula.

WAATHIRIKA WAKUBWA WA TATIZO LA UPUNGUFU WA VITAMINI A NA MAAMBUKIZI YA MINYOO NI AKINA NANI?
· Watoto wadogo huathirika zaidi na tatizo la upungufu wa vitamin A na maambukizi ya minyoo kutokana na sababu mbalimbali. Aidhaa wanawake wajawazito huathirika zaidi na tatizo la upungufu wa vitamin A.
· Watoto wanahitaji vitamin A kwa ukuaji na maendeleo mazuri na kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali ya utotoni, upungufu wa vitamin A kwa watoto unaweza kusababishwa na ulaji duni ikiwa ni pamoja na kutonyonya vizuri maziwa ya mama, kuwalisha watoto vyakula vya nyongeza visivyokuwa na vitamin A kwa wingi au maziwa mbadala wa maziwa ya mama, kuwaachisha watoto kunyonya maziwa ya mama mapema kabla ya kutimiza umri wa miaka miwili, kiwango kisichokidhi cha vitamin A kwenye maziwa ya mama kutokana na lishe duni na maambukizi ya maradhi,
· Watoto wenye umri chini ya miaka mitano hupata maambukizi ya minyoo mara kwa mara kutokana na tabia ayao ya kucheza kwenye kwenye udongo na mazingira machafu.
· Wanawake wanahitaji vitamin A mwilini kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa mimba. Pia wanahitaji vitamin A mwilini ili kuboresha hali ya vitamin A ya mama anayenyonyesha.


Your reaction?

1
LOL
0
LOVED
0
PURE
0
AW
0
FUNNY
0
BAD!
0
EEW
0
OMG!
0
ANGRY
0 Comments